Skip to main content
Wanasheria Wa Amina Khalef @aileenalora (Mke wa @officialalikiba ) Wamemtaka Diamond Platnumz ndani ya Siku saba aombe hadharani Msamaha Baada ya Kumchafua Mteja Wao Amina Khalif. Hivi karibuni kulikuwa na Utani Unaondelea Mtandaoni kati ya Ali Kiba na Diamond Platnumz, katika Utani huo @diamondplatnumz aliandika "Habari yangu na Amina nadhani unayo..." Maana ya Maneno hayo kwa Mujibu wa Wanasheria wa Amina wanadai kwamba Diamond Platnumz alimaanisha kuwa amewahi kuwa na Uhusiano na Amina. Wanasheria wanadai Maneno hayo sio ya Ukweli,Amina Ni Mwanamke ambaye anajiheshimu na hajawahi kukumbwa na Skendo mbaya. Wanasheria Wameeleza kwamba Kauli hiyo kutoka Kwa Diamond Platnumz Imeshusha Heshima ya Amina,kwa Sasa anajisikia Vibaya,bahati mbaya zaidi jambo hilo limeathiri mpaka Marafiki,Ndugu,jamaa na marafiki wa Amina. Wanasheria wanaomba Diamond Platnumz Aombe Msamaha na akanushe Ujumbe wake ndani ya Siku Saba,Akishindwa kufanya Hivyo hatua zaidi za Kisheria zitachukuliwa Dhidi yake. Credit by @Presenterdax Tafadhari tembelea YouTube channel yetu ya Presenter dax kwa taarifa nyingi zaidi.
Popular posts from this blog
Comments
Post a Comment